Safari ya zena Ep 01

 



Jina la simulizi:

SAFARI YA ZENA

Sehemu ya 1

Mwandishi: YOUNG NDABA DE LILIAN

Website: mastorihub.blogspot.com



---


"Ijapokuwa huzuni kitakapopita kicheko, umasikini ukiweka kambi katika malango yako. Ama pepo la utajiri likikupitia, iwe kwa ugumba ama kwa maradhi mshukuru yeye aliye juu. Maana yeye, Anajua kwa nini anakupitisha katika hayo, hakuna jambo linalokuja kwa akili zako mwenyewe, usijikweze."


Maneno haya yaliandikwa kwa kalamu ya imani na yamebaki yakiwa ya dhahabu moyoni mwa Zena tangu alipokuwa msichana mdogo kule kijijini Mwembechai, Tandahimba. Yalikuwa ni maneno ya bibi yake, Bibi Rukia, ambaye licha ya uzee na maradhi, alikuwa na macho yaliyoona mbali zaidi ya wengi waliokuwa na afya njema.


Zena alizaliwa kwenye familia iliyojitahidi kupambana na maisha kwa kila njia. Alikuwa binti wa mwisho kwa mama yake, Halima, ambaye aliuza maandazi na samaki kwa muda mrefu sokoni. Baba yake, Ramadhani, alifariki dunia alipokuwa na miaka mitano. Hivyo maisha ya Zena yalimlea katika nyanja zote za mapambano, subira, na imani.


Miaka ikasonga.


Zena alipata elimu ya sekondari kwa shida na mshindo wa maombi. Kisha akaja Dar es Salaam kwa matumaini ya kupata kazi au angalau maisha bora zaidi. Lakini jiji halikuwa na mikono ya huruma kama alivyotegemea. Alihangaika. Alilala kwa rafiki zake, akiuza urembo mitaani, na mara nyingine akiuza kanga na sabuni.


Lakini ugumu halisi ulianza alipoambiwa hana uwezo wa kuzaa. Taarifa hiyo ilimvunja moyo, lakini haikumbadilisha roho yake. Aliendelea kumshukuru Mungu katika kila hatua, akisema:


"Huenda nina watoto wa kiroho ninaopaswa kuwalea kwa hekima. Mungu hajakosea."


Ndipo siku moja, akiwa amevunjika kabisa, akiwa hana nauli wala matumaini ya chakula cha usiku, alisimama mbele ya Crown Hotel—baaa ya kifahari katikati ya jiji la Dar.

Pumzi ya harufu ya kahawa, shisha na pombe ya mvinyo ilimkaribisha ndani kana kwamba kulikuwa na sauti ya siri iliyomwita.


Ndani ya baa hiyo alikutana na watu wa kila aina: walioshinda, waliopotea, waliojificha, na waliokuwa wakitafuta nuru. Lakini hapo ndipo alikutana na mtu ambaye hakuwa wa kawaida—Mama Mariam, mwanamke mzee aliyekuwa ameketi peke yake, akisoma Biblia huku akiwa na tasbihi mkononi.


“Unatafuta nini hapa, mwanangu?” aliuliza Mama Mariam, kwa sauti ya utulivu yenye mamlaka ya kiroho.


Zena hakuweza kujibu kwa haraka. Machozi yalimtoka.


Ndipo Mama Mariam alipoanza kumweleza kuhusu maisha, imani, na majira ya Mungu. Alimwambia, "Kila mtu aliye hapa si kwa bahati mbaya. Wewe ni zawadi ya kipekee katika giza hili. Na mwanga wako utaangaza siku moja—kama hutakata tamaa."


Kuanzia siku hiyo, Zena alianza safari mpya. Alianza kuhudhuria vikao vya maombi vilivyoendeshwa chini ya ghorofa ya Crown Hotel. Akaanza kusaidia wasichana waliopotea njia.


Na licha ya kuwa bado hana mtoto wa kuzaa, alikuwa mama wa wengi waliopata mwelekeo mpya kupitia hekima yake.



---


🌟 "Kila giza lina chanzo cha mwanga—usiache kutafuta kibali cha kiroho katika magumu yako." 🌟


ITAENDELEA.... ✨🕊️


Maoni